NDOA NA FAMILIA
Je ndoa ya wake wengi ni halali kibiblia?
Katika biblia kuna kumbukumbu za watu kuoa wake wengi, mfano Yakobo alikuwa na wake wanne, Sulemani mia saba na wengine wengi. Na Yesu alikuja kusema kuwa mke ni mmoja na mume mmoja, je kuna uthibitisho mwingine wa kutosha kwenye biblia kuthibitisha kuwa ndoa za wake wengi ni halali?, naomba tujadili hili..
Biblia inaruhusu kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine
Kuna watu wa imani nyingine tofauti na Ukristo ambao kimsingi ni wenye adabu na staha sana, na wengine wanafaa kuwa wake au waume zaidi hata ya baadhi ya wakristo, Je ikitokea nimempenda mmoja na ninaweza kufunga naye ndoa?
Tukikumbuka kuwa kwenye biblia alikuwepo Boazi aliyemwoa Ruthu mwanamke wa Taifa lingine na mambo yalikwenda vizuri tu!, kwanini sasa isikubaliwe?
Kuachana ni dhambi?
Mfano mke wangu ameanza kukosa adabu, haniheshimu tena kama zamani, na ananisaliti, tumejaribu kutafuta suluhisho kwa viongozi wa dini na wazazi wa pande zote lakini imeshindikana, zaidi sana yeye mwenyewe anataka tuachane, je nikimwacha huyu na kuoa mwingine nitakuwa natenda dhambi..
Na maana yake nini Yesu aliposema "amwachaye mkewe isipokuwa kwa habari ya uasherani azini" alikuwa na maana gani, maana naona ni kama kuachana kumeruhusiwa hivi, lakini katika condition fulani fulani hivi kama hizo za uasherani.. hili tulijadili jamani!
- 15 Forums
- 7 Topics
- 8 Posts
- 0 Online
- 15 Members