Injili Forums Forum
Je ndoa ya wake wengi ni halali kibiblia?
Katika biblia kuna kumbukumbu za watu kuoa wake wengi, mfano Yakobo alikuwa na wake wanne, Sulemani mia saba na wengine wengi. Na Yesu alikuja kusema kuwa mke ni mmoja na mume mmoja, je kuna uthibitisho mwingine wa kutosha kwenye biblia kuthibitisha kuwa ndoa za wake wengi ni halali?, naomba tujadili hili..
Biblia inaruhusu kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine
Kuna watu wa imani nyingine tofauti na Ukristo ambao kimsingi ni wenye adabu na staha sana, na wengine wanafaa kuwa wake au waume zaidi hata ya baadhi ya wakristo, Je ikitokea nimempenda mmoja na ninaweza kufunga naye ndoa?
Tukikumbuka kuwa kwenye biblia alikuwepo Boazi aliyemwoa Ruthu mwanamke wa Taifa lingine na mambo yalikwenda vizuri tu!, kwanini sasa isikubaliwe?
Kuachana ni dhambi?
Mfano mke wangu ameanza kukosa adabu, haniheshimu tena kama zamani, na ananisaliti, tumejaribu kutafuta suluhisho kwa viongozi wa dini na wazazi wa pande zote lakini imeshindikana, zaidi sana yeye mwenyewe anataka tuachane, je nikimwacha huyu na kuoa mwingine nitakuwa natenda dhambi..
Na maana yake nini Yesu aliposema "amwachaye mkewe isipokuwa kwa habari ya uasherani azini" alikuwa na maana gani, maana naona ni kama kuachana kumeruhusiwa hivi, lakini katika condition fulani fulani hivi kama hizo za uasherani.. hili tulijadili jamani!
Kaini alimwoa nani
Kaini alilaaniwa na hatujui alienda kumwoa nani lakini tunasoma alizaa watoto tena hodari tu, sasa alizaa na nani au kulikuwa na mwanamke mwingine tofauti na Hawa?
Biblia halisi ina vitabu vingapi
Wengine wanasema ina vitabu 66, wengine vitabu 73 wengine vitabu 88 na wengine zaidi ya mia... Binafsi naamini inavyo 66, lakini nataka nipate uhakika zaidi juu ya hili, kwasababu tumezaliwa tu na kuambiwa hivi sisi wenyewe hatufanya uchunguzi... sasa tusaidiane kidogo hapa..
Rangi ya Biblia inajalisha sana?
Wana jukwaa nimekutana na watu wanadai eti, biblia ikiwa nyeusi haina nguvu ya Mungu, na ni makosa kutumia biblia yenye kava la rangi nyeusi, na pia yenye msalaba, biblia inatakiwa iwe nyeupe sasa huu ni ufunuo mpya kwangu, lakini napenda kusikia maoni zaidi, tusije tukapotea.
Huu mtindo wa uvaaji kunani?
Jamani huu mtindo wa wanawake kuingia kanisani maziwa yakiwa yanaonekana na hata mgongo ukiwa wazi na vijana kupiga modo halafu na kiduku kichwani ni sawa kweli?
Mafuta ya upako.
Haya mafuta ya Upako,chumvi na maji siku hizi kila mahali yapo, tujadiane kama ni sahihi kutumia maana yalianza kama mshtuko kwa majority lakini sasa ni kama yamekubalika sio tena kitu cha kushangaza, ni kama tumelazimishwa kuamini na tumekubali..
Kanisa la kweli ni lipi duniani
Nafutailia kujua kanisa la kweli ni lipi, ila bado sijalipata, Kwanza nitajuaje kanisa la kweli kwasababu yapo mengi na kila siku yanaongezeka, na yana majina tofauti tofauti.. lakini kwa imani ya wenzetu hakuna migawanyiko mingi kama ya kwetu... kuna nini huku?.. tufuate lipi?
Mistari ya faraja
Ni mistari gani ya Biblia inafaa wakati wa misiba au wakati wa matatizo megine?
Wapo malaika wanaoweza kulala na watu na kuzaa nao watoto?
Kitabu cha Henoko kinasema wale wana wa Mungu ni malaika walioshuka na kulala na wanawake wa kibinadamu, wakazaa nao watoto, sasa labda naweza kukubali, lakini nauliza na leo malaika walio mbinguni wanaweza kushuka na kulala na watu, kama mapepo yanavyofanya sijui nimeeleweka.
kuna malaika wangapi mbinguni.
Kuna Malaika wangapi mbinguni, na kazi zao ni zipi na majina yao kama kuna mwenye elimu hiyo ila tusidanganyane. Tutoe na uthibitisho wa biblia
Kunyakuliwa ni kabla au baada ya ile dhiki kuu?
Kuna hii ishu ya unyakuo, naitaji sana kujua ukweli wake ni upi hasaa.. Tutanyakuliwa kwanza ndio dhiki kuu itakuja (kama walokole wanavyoamini) au dhiki kuu itakuja kwanza ndipo tunyakuliwe baadaye (kama wasabato wanavyoamini).
Naomba nijibiwe kwa hoja za kibiblia si kidini.
Pia linganisha mistari hii Mathayo 24:29-31 na 1Wathesalonike 4:13-18
Naota misiba misiba nini maana yake?
Haipiti wiki mbili sijamwota mtu aliyekufa, kuna wakati hizi ndoto zinapotea ila kuna wakati zinarudi kwa kasi, yaweza kusababishwa na nini au zinaashiria nini,,
- 15 Forums
- 7 Topics
- 8 Posts
- 0 Online
- 15 Members