Shimo la moto la Darvaza au maarufu kama “Lango la Kuzimo la Darvaza” ni shimo kubwa ambalo limekuwa likiwaka moto kwa zaidi ya miongo mitano mfululizo (miaka 50) bila kuzimika.
Bonde hili lipo kwenye Nchi ya Turkmenistan, iliyopo Asia ya Kati, kwaasili
Shimo/bonde hili lilitokeaje?
- Mnamo mwaka 1971, wataalamu wa Kisovieti walikuwa wakichimba gesi asilia.
- Ardhi iliporomoka ghafla, ikaunda tundu kubwa lenye kipenyo cha zaidi ya mita 70.
- Gesi ya methane ilianza kutiririka kwa kiwango kikubwa.
- Ili kuzuia gesi yenye sumu kusambaa, wataalamu waliamua kuwasha moto ili iungue.
- Walidhani moto utazima baada ya siku chache…Lakini umewaka kwa zaidi ya miaka 50 bila kuzimika!
Maajabu yake (Jambo la kushangaza)
1. Moto haujawahi kuzimika kwa miongo kadhaa
Moto huo umewaka mfululizo tangu 1971—zaidi ya miaka 50.
Hii ni ajabu kwa sababu:
- Methane huisha haraka kawaida
- Lakini hapa inatoka muda wote kutoka ardhini
2. Mwanga wake unaonekana mbali sana jangwani
Usiku, mwanga wa shimo hilo unaonekana kama jua dogo linalowaka katikati ya jangwa.
3. Ni tundu kubwa lenye moto mkali
- Kipenyo: ~70 mita
- Kina: ~30 mita
- Joto juu ya krateri ni kali sana, karibu na 800–1000°C
4. Haiwezi kuzimwa kirahisi
Serikali ya Turkmenistan ilijaribu kupanga kuzima ili kupunguza upotevu wa gesi, lakini:
- Moto hauzimiki
- Gesi bado hutoka kwa nguvu
- Hatari ya milipuko ipo ikiwa wataiziba kwa nguvu
🔥 Kwa nini huitwa “Lango la kuzimu/ The Door of Hell”?
- Inaonekana kama mlango wa kuzimu kwasababu
- Moto unawaka daima bila kukoma
- Kuna joto kali na mwanga wa kutisha
- Usiku, mwanga wake huonekana maili nyingi mbali na jangwa
Kwa macho ya kawaida, inaonekana kama:
“shimo la duniani linaloongoza kwenye moto wa chini”

SHIMO HILI LINAHUBIRI NINI KIROHO?
Ni wazi kuwa linahubiri kuwa lipo shimo mfano wa hilo MAHALI PENGINE lenye moto usiozimika..
Kama wanadamu wanaweza kuunda shimo lenye moto usiozimika ni lazima ipo nguvu nyingine yenye uwezo zaidi ya wanadamu, yenye kuumba mfano wa hilo, na lenye ukubwa zaidi ya huo..
Marko 9:45-46 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”
Ziwa la Moto lipo! Na Yesu anarudi.


