
Biblia ni Neno la Mungu lililoandikwa. Hiki ni chanzo halisi cha uongozi kwetu wote. Neno la Mungu ni sauti isiyosikika.
Jinsi gani sauti iwe isiyosikika? Sauti zisizosikika ni kundi la sauti ambazo Roho Mtakatifu anazitumia katika kutuongoza.
Hazisikiki kwa maana ya kwamba huwezi kusikia mtu akiongea kwa sauti ya kusikika. Hata hivyo, sauti hizi ni njia za kawaida ambazo Roho Mtakatifu huzitumia kwa kutuongoza sisi sote.
Unaona, kuongozwa na Roho Mtakatifu si jambo jepesi sana. Leo, wanadamu huwasiliana kwa kuongea, kugusa, kujieleza kwa uso, kwa barua, nukushi, simu, luninga, barua pepe, n.k. Pia kuna utaratibu ambao Mungu huwasiliana na watoto wake. Moja ya njia hizo ni Neno la Mungu lililoandikwa.
Neno la Mungu
Neno la Mungu limetolewa kwetu kwa ajili ya uongozi wa maisha yetu. Kila kitu tunachokifanya lazima kifanyike kulingana na Neno la Mungu. Kwa ujumla wake, Neno la Mungu ni kitabu kamili cha mwongozo kwa maisha yetu. Biblia ni
kitabu cha kipekee chenye maelekezo kwa kila jambo linaloweza kutokea. Kuna watu wengi wanaofikiri kwamba Biblia si kitabu kinachohusika na utendaji kwa siku za leo.
Mwanamke mmoja aliniambia kwamba aliamini angeweza kufanya uzinzi kwa sababu Biblia imepitwa na wakati.bBaada
ya miaka mitatu, wakati mpenzi wake alipomtelekeza, ndipo alitambua kwamba Biblia ilikuwa si kitabu cha zamani kuliko
vyote.
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
2 Timotheo 3:16,17
Maandiko yana manufaa, yana matokeo, yanahusika na utendaji kwa kila Mkristo leo! Kuna Wakristo wengi ambao hawataki ufungue Biblia; wanataka tu unabii au neno la maarifa.
Neno ni Nuru
…Na taa nimemtengenezea masihi wangu. Zaburi 132:17
Tumia neno la Mungu kama mwanga wa njia yako. Katika ulimwengu kuna giza nene. Mara zote hatujui mambo ya
kufanya, lakini Mungu ametoa nuru kwa Wakristo. Nuru hii ni nini ambayo Mungu ametoa kwa Wakristo?
Neno lako ni taa ya miguu yangu,na mwanga wa njiayangu. Zaburi 119:105
Neno la Mungu ni taa na mwanga kwetu. Utajua unakoenda ikiwa tu utawasha mwanga. Ikiwa utawasha mwanga ndipo hutajikwaa katika samani za nyumbani. Yesu Kristo alijiita ni mwanga wa ulimwengu huu.
…Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yauzima. Yohana 8:12
Unahitaji nuru katika maisha haya! Yesu (Neno) ni nuru kwa maisha yako. Watu wanaojaribu kuishi bila kuwa na Kristo na Neno wamegundua kwamba kuna maumivu unapojikwaa katika giza.
Neno ni Hekima
Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu …Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Zaburi 119:98, 99
Neno la Mungu litakufanya mwenye hekima katika maisha haya. Ushauri na uongozi wa biashara vinapatikana katika Neno la Mungu. Katika Neno la Mungu kuna maagizo mengi zaidi kwa mfanyabiashara kuliko mhadhiri wa chuo katika utawala wa biashara. Kuna ufahamu unaohusika na utendaji juu falisafa, sayansi ya siasa, fasihi na historia katika Biblia kuliko katika kitabu chochote ninachokifahamu.
Neno ni Maelekezo
Wakati mwingine hutabasamu watu wanaposema, “Mungu ameniita nifanye hili na lile kwa ajili yake.” Ikiwa hutii maelekezo mepesi katika Neno, unadhani Mungu atakupa zaidi?
Aliyemwaminifu katika lililo dogo, atakuwa mwaminifu hata katika lililo kubwa.Ikiwa hutii Neno la Mungu linalosema juu ya kutoa fungu lako la kumi,unadhani Mungu ataongea kwako kuhusu huduma ya muujiza wa uponyaji.
Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema, na BWANA anataka nini kwako…..Neno Huleta Ufahamu
Katika siku za mwisho, Mungu anatoa wachungaji ambao watatulisha kwa maarifa na ufahamu. Pokea maarifa na ufahamu ambao Mungu anakupatia.
Nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo
wangu, watakaowalisha kwa maarifa na ufahamu.
Yeremia 3:15
Pia Mungu atawatumia watu wa Mungu kukupa maelekezo kwa maisha yako. Maelekezo haya yatakusaidia uwe mtu bora. Kuna wakati ambao mchungaji wako atakuamrisha ufunge na kuomba. Ni jambo la maana kufuata maagizo haya. Biblia inatufundisha kwamba tunatakiwa kuwatii wale wenye mamlaka ya kiroho juu yetu.
Watiini wenye kuwaongoza, maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu …
Waebrania 13:17
Sikiliza sauti ya mchungaji wako. Mungu aliagiza hatima ya kondoo kwa mchungaji. Mungu atabariki maisha yako na kukuongoza kupitia sauti ya mchungaji wako. Yesu ndiye mchungaji mkuu na alimwambia Petro kuchunga kondoo. Hiya ina maana kwamba aliagizia utunzaji wa kondoo wake uwe chini ya mchungaji.
…Simoni mwana wa Yohana wanipenda?..Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
Yohana 21:17
Sauti ya Mchungaji
Kwa kuwa mchungaji anaongea Neno la Mungu, sauti ya nchungaji ina nuru, ufahamu na hekima unayoihitaji.
Ikiwa wewe ni kondoo, Mungu atakuongoza kupitia mchungaji wako. Mara unapofanana na kondoo utapokea uongozi kutoka kwa mchungaji wako. “Kondoo wangu wanaijua sauti yangu na kunifuata.” Mchuganji wako atakuelezea mafundisho yote kuhusu Biblia. Unatakiwa uwe makini kwa maneno anayokuambia mchungaji wako. Ni maneno ya mchungaji yaliyopakwa mafuta kwa ajili ya kondoo. Maneno hayo yamebeba uongozi wote ambao kondoo wanahitaji.
BWANA akubariki sana.
Kwaushari zaidi wa Neno la Mungu lenye uzima wa milele wasiliana nasi kwa. No. 255 782044449/255 740444132